Sale!
Duration:
Siku Tatu
Transport:
Gari la kitalii la 4 x 4 rufu ya kunguka juu
Tour Type:
Safari za Siku
SKU:
Bei ni kwa Siku kwa Mtu Mmoja Tshs 142,000/=
Group size:
kuanzia watu 4 hadi 50
Location:

Siku 3 za safari Porini na ATA Safaris

$560,000.00 $425,000.00

Siku za za Safari na kampuni ya ATA Safaris itageuza kabisa mtazamo wa faham katika maisha na kukufanya kufikiri upya kama si kuwa kuwa mtu mpya kifikra, hebu fikiri watalii wanasafiri kutoka nchi za mbali kuja kushangaa maajabu yaliyopo Tanzania ambayo hayapo sehemu ingine Duniani na sisi ni watanzania tumezaliwa hapa na tunapewa bei nafuu zaidi ya upendeleo.

karibu tukupeleke kisha utashangaa vile Tanzania ilivyo nzuri …

 

wws Maya / Pre-sale Questions Need Help? Contact Us via WhatsApp
Departure:
Total: 425000
SKU: Bei ni kwa Siku kwa Mtu Mmoja Tshs 142,000/= Category: Tags: , , , , , ,
Discount:

Special offer

Description

Kwa mara ya kwanza kabisa ATA Safari .. wakala wa safari duniani pote wanakuletea safari za ndani kwa lugha yetu hadhimu ya kiswahili.

Safari hizi zitaanzania Arusha , kwa hivyo kwa watu wanaotokea mikoani tunaweza kuandaa tiketi za mabasi ama treni ili  kufika Arusha, pia kwa wale wenye usafiri binafsi basi tunaweza kuandaa hotel za bei Nafuu ambazo zitajumuisha milo yote pia kwa bei nafuu.

Bei zetu ni kwa watanzania na zitalipwa kwa njia ya pesa za kitanzania kupitia Account zetu za kampuni.

MPANGO WA SAFARI:

SIKU YA MMAPOZI:

Waongoza wageni wa kampuni ya ATA watawapokea ikiwa mmetokea mkoani na kuwapeleka kwenye Hotel kwa ajili kulala na kula kisha kupumzika kwa siku inayofuata, bei itajumuishwa kwenye fungasho la bei utakayopewa hapo chini.

Kwa ale wataopenda kufanyiwa utaratibu wa kufika Arusha ATA itawasiliana nao na kisha kuweka taratibu kwa mawasiliano na bei pia itajumuishwa kwenye fungasho la bei utakayopewa hapo chini.

Kwa wale waliopo Arusha ama kuanzia Arusha basi wafanyakazi wa ATA  watawasilina na kuweka taratibu za kukutana nao siku moja kabla ya kuanza safari.

SIKU YA KWANZA: ARUSHA KWENDA NGORONGORO.

Waongoza wageni wa ATA Safaris watawachukua wageni wetu kutoka Hotelini/ ama mahala walipotaarifiwa kufika na kuanza Safaris wakiwa chakula pamoja na box za maji zilizohifadhiwa kwa ubora wa kitalii.

Siku hii tunaitembelea Ngorongoro Crater Mambo Muhimu kabisa .. tutashuka shimoni (crater ) kwa zaidi ya masaa sita chini kutalii ikiwa ni pamoja na kupata chakula cha mchana tukiwa ndani ya shimo la ngorongoro (The Ngorongoro Crater)

Tutapata nafasi pia kutembelea ziwa lililopo shimoni na kuangalia wanyama tofauti wakiwamo Simba, Chui, Tembo , viboko, Twiga na wengineo wengi.

Muda wa Jioni tutaanza Safari kurudi katika Hoteli iliyopo katika eneo la Manyara ama Mto wa Mbu kwa ajili ya kulala na kupumzika kusubiri siku inayofuata. chakula na malazi vitajumuishwa hapa.

SIKU YA PILI: KUTEMBELEA  HIFADHI YA MANYARA:

Siku ya leo tutatembelea Hifadhi ya Manyara siku hii tutaondoka na boksi xa chakula pamoja na maji kutoka hotelini kwenda hifadhini  ambapo pia kuna ziwa Manyara hapa tupo katika bonde la ufa, tutatembelea ziwani na kwenye Hifadhi kujionea wanyama tofauti na kutembelea pia chemichemi za maji moto . hapa ni mahali ambapo tunaweza kuona simba wapanda miti ambao ni sehemu hii tu duniani wanapatikana pamoja na wanyama wengine wengi na wazuri.

Tutakuwa na siku nzima porini kisha jioni tutarudi hotelini kupumzika na kulala kuisubiri siku inayofuata. Chakula na malazi vitajumuishwa katika kifungashio cha bei zetu.

SIKU YA TATU – KUTEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE:

Siku ya leo tutatoka hasubuhi na mapema baada ya Chai Hotelini na tutasafiri kwenda hifadhi ya Tarangire ambayo ipo pia jirani na hifadhi ya Manyara… hapa tutaondoka na box za chakula pamoja na maji kutoka hotelini na tutakuwa siku nzima ya utalii katika hifadhi pendwa ya Tarangire.

Katika hifadhi hii tutajionea wanyama wenye maumbile makubwa zaidi, tembo wale wakubwa, mbogo, simba na wengineneo wakiwamo ndege wakubwa kama mbuni, ikiwa mazingira ya hali ya hewa yatakuwa rafiki tunaweza kutembelea eneo la silalei ambapo tunaweza kuona njoka wakubwa kama cobra, chatu nk.

Jioni dereva wetu atawarudisha wageni wetu katika jiji la Arusha ambapo utakuwa ndio mwisho wa safari. utarudishwa hotelini kama ulichukuliwa hotelini ama kwenye eneo ambalo ulichukuliwa ikiwa wewe ni mkazi wa eneo la Arusha.

 

 • BEI TSHS NI 425,000/= KWA SIKU KWA MTU
 • GROUP YA KUANZAIA WATU WATANO.

UJUMUISHO WA KIFUNGASHIO CHA BEI:

 • Dereva mtaalamu wa uongozaji wa wageni.
 • Usafiri Gari lenye hadhi ya kitalii aina ya Land cruiser/ Land rover Jeep – (pop up roof proffessional for safari)
 • Chakula  na malazi siku zote za Safari
 • Chupa ya maji kwa kila msafari katika siku za safari.
 • Viiingilio katika hifadhi za wanyama.
 • Viingilio katika shimo la Ngorongoro
 • Hotel siku ya kwanza kwa wageni wa nje ya Arusha. (Chakula na malazi)

KIFUNGUSHIO HAKITOJUISHA YAFUYO

 • Gharama za vinywaji katika Hotel
 • Gharama za ufuaji wa nguo katika hotel
 • Gharama nyinginezo ambazo haziko katika ujumuisho wa kifungashio cha bei.
 • Gharama za Bima endapo kutatokea hatari ya Barabarani.
 • Gharama za mawasiliano ya Simu wakati wa safari.***
 • Gharama za Hotel baada ya Safari,
 • Ggarama za kufika Arusha kwa wale walio nje ya Mkoa wa Arusha.